Chakula Cha Mchana Pamoja Na Watoto wa Mtaani.
Chama
cha skauti Tanznaia kupitia wilaya ya ilala mkoani Dar Es Salaam
wameanziasha program ya kula chakula cha mchna pamoja na watoto wa
mitaani kila wiki, kwa lengo la kuwavuta karibu ili kuwasadia kuondokana
na maisha wanayo ishi sasa kwa kuwatafutia fursa mbalimbali zitakazo
waendeleza kimaisha na hatimae waje kuwa wazazi bora katika familia
zao.
Kamishna wa skauti (w) ilala akifanya mazungumzo na watoto wa mtaani na kuwafanyia usjili. |
vijana wa mtaani wakisikiliza mongezi kutoka kwa kamishna wa wilaya ya ilala |
Vijana wa skauti mkoa wa Dar es salaam wakibadilisahna mawazo na wageni wao (watoto wa mtaani) |
Kamishna
msaidizi wa wilaya ya ilala Bw. Peater Powel akiwanasihi vijana wa
mitaani pamoja na vijana wa skauti juu ya athari za kujiweka katika
makundi yasiyo faa. |
Skaui wakiwahudumia chakula vijana wenzao washio mitaani kama tafrija ya kukutana kwao kila wiki. |
Skaui wakiwahudumia chakula vijana wenzao washio mitaani kama tafrija ya kukutana kwao kila wiki. |
Vijana wakiwa katika wakati eneo la skauti upanga (makao makuu ya skauti Tanzania) wakipata chakula cha mchana na skauti. |
|
Ilala District Local Scout Association
Have Lunch with Ilala Scout together with Street Children
Alhamisi, 3 Julai 2014
MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI DUNIANI. THEME ‘‘Right of Peoples to Peace”
SIKU YA KIMATAIFA YA AMANI DUNIANI
Siku ya Kimataifa ya Amani Duniani ni siku iliyopangwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kukomesha vita, kutoa elimu juu ya amani na kuimarisha haki za binadamu ambayo husherehekewa tarehe 21 Septemba ya kila mwaka.Mwaka huu 2014, Skauti (Tanzania) tutaungana na Mataifa mengine ya Dunia katika kusherehekea siku hii muhimu ikiwa imebeba kaulimbiu isemayo, ‘‘Right of Peoples to Peace”
Lets meet to the summit of Mt. Kilimanjaro with the Peace message.Mh. Abdulkarim Shah (Mb) Kamishna mkuu Chama Cha Skauti Tanzania. |
Utaratibu wa Upandaji Mlima:
Umri:
> Skauti watakaoruhusiwa kupanda Mlima Kilimanjaro ni wale walio na umri wa miaka 12 na kuendelea, wavulana, wasichana na viongozi wao.
Afya:
> Kila mshiriki atahitajika kupima afya yake katika kituo chochote cha afya kujihakikishia kuwa na afya bora kabla ya kupanda mlima.Vifaa vya Kubeba
> Vifaa vya usafi:- Sabuni ya kuogea, sabuni ya kufulia, mswaki, dawa ya mswaki, mafuta ya mgando n.k.
> Mavazi:- Nguo nzito za baridi Masweta, jackets, nguo za michezo, soksi za mikono na miguu, kofia za baridi n.k.
Ada ya Ushiriki:
> Kila mshiriki atawajibika kuchangia kiasi cha Tshs. 150,000/= ambayo itajumuisha gharama za kuingia mlimani, gharama za kupanda mlima, chakula na malazi kwa kipindi chote cha siku za kupanda mlima.
> Gharama nyingine za usafiri kutoka na kurudi katika mikoa husika na ada za kutoka nje ya mikoa zitagharamiwa na mshiriki mwenyewe binafsi.
> Malipo ya kila mshiriki yanahitajika kulipwa kupitia Akaunti ya Chama cha Skauti Tanzania, iliyoko katika Benki ya National Bank of Commerce (NBC) tawi la Samora,
Account Number 012103010625. Baada ya malipo, Makamishna wa Mikoa watawajibika kutuma majina ya Skauti watakaolipa na namba za stakabadhi za malipo ya Bank Makao Makuu ya Chama kwa uthibitisho.
Kuthibitisha Ushiriki:
> Washiriki watahitajika kuthibitisha ushiriki wa kupanda Mlima kwa Kujaza fomu na kuirejesha Makao Makuu ya Chama cha Skauti Tanzania kwa njia ya barua pepe (Email) kabla ya tarehe 18 Julai 2014 au kupitia kwa Makamishna wa Mikoa.RATIBA:
S/No. TAREHE TUKIO MUHUSIKA
1. 16 - 17 Septemba 2014 Kuwasili Mkoani Kilimanjaro Uongozi wa Skauti Mkoa wa
Kilimanjaro na Uongozi wa
Skauti\ Makao Makuu.
2. 18 - 21 Septemba 2014 Kuwasili Kileleni mwa Mlima Skauti wapanda Mlima
Kilimanjaro
3. 22 Septemba 2014 Kurejea chini ya mlima Skauti wapanda Mlima
4. 23 Septemba 2014 Kuondoka Kilimanjaro Skauti wote
Ni mategemeo yetu kuwa Skauti tutajitokeza kwa wingi kuonyesha mshikamano wetu katika kupeleka ujumbe wa Amani kwa njia kupanda mlima wetu Kilimanjaro, Mlima mrefu Barani Afrika wenye kuleta Amani, Upendo na Matumaini pale ambapo hakuna matumaini
Kwa maelezo zaidi kuhusu upandaji mlima, na watakao hitaji fomu za ushiriki {kwenda kusherekea siku ya Amani duniani} tafadhali tutumie ombi hilo la kupata fomu hiyo kupitia :
Mobile: +255 713 295 715
Tell: +255 2222 153342
Fax: +255 2222 1248 807
Email: Tanzani Scout Association
![]() |
MLIMA KILIMANJARO |
![]() |
Alhajj. Omar Khatib Mavura Mratibu Messengers of Peace Taifa. |
Murtadhwa Rashid Abdallah Mratibu Messengers of Peace Mkoa (Dar-es-salaam) |
https://www.facebook.com/pages/Messengers-of-Peace-Tanzania-MOPTZ/1408726232704353?ref_type=bookmark
HATIMAE JUKWAA LA VIJANA LAPATA WAJUMBE WA KAMTI KUU TANZANIA. {TANZANIA YOUTH COMMITTEE} 2014-2016
JUKWAA LA VIJANA TANZANIA, {TANZANIA YOUTH FORUM} 28-30 JUNE,2013 BAHATI CAMP-MOROGORO.
Chama cha Skauti Tanzania chapata uongozi mpya wa jukwaa la vijana
"Youth Forum" yenye wajumbe sita (6) chini ya mwenyekiti Bw. Chacha N.
Mwita ambae amekabithiwa rasmi jukumu hilo mapema wiki hii baada ya
kuchaguliwa na na vijana walioshiriki jukwaa hilo kutoka mikoa tofauti
iliyopo nchini Tanzania, uchaguzi huo uliofanyika 28-30 june, 2014
sambamba na kuendeshwa kwa kongamano hilo juu ya maendeleo ya uskauti na
vijana wa skauti kiujumla.
![]() |
Timu iliyoshiriki jukwaa la vijana |
Aidha nae Bw. Chacha (baada ya kuchaguliwa kwa nafasi hiyo) aliitaka kamati yake kuwa makini na kuwa tayari kukitumikia chama cha Skauti Tanzania (kwa kutumia nyadhifa walizo nazo kama viongozi wa vijana nchini) kwa hali na mali ili kuhakikisha wanafikia malengo na dhamira ya chama cha Skauti kidunia.
Pia Bw. Chacha (Mwenyekiti) alitoa wito kwa vijana wa skauti nchini
(Tanzania) kuonesha na kuwapa ushirikiano wanakamti hiyo ya jukwaa la
vijana la Tanzania iliyoundwa 30 june, 2014 ili kufanikisha utendaji wa
kamati hiyo.
Vile vile Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani) alisisitiza juu ya ushirikiano wa vijana (skauti) na kamati hiyo ili kuleta manufaa kwa wana chama (skauti) katika nche yetu na ulimwengu kiujumla.
Ndugu katibu
mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani Bw.
Murtadhwa R. Abdallah aliwaeleza kwa upana zaidi wajumbe walio hudhuria
kongamano hilo juu ya masuala ya ujumbe na wajumbe wa amani (Semina
fupi elekezi) na kuwataka wajumbe hao waliohudhuria kongamano hilo kuwa
wajumbe (mabalozi) wa kulifikisha na kulifanyia kazi suala la ujumbe na
wajumbe wa amani katika mikoa yao na kuanza kulifanyia kazi kwa vitendo
suala hilo.
![]() |
Ndugu. Murtadhwa R. Abdallah (katibu mkuu wa jukwaa la vijana nchini, pia ni mratibu wa wajumbe wa amani) |
Sambamba
na viongozi hao wa jukwaa la vijana, pia Kamishna mkuu msaidizi Mwl.
Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini) aliipa baraka
kamati hiyo ya jukwaa la vijana nchini na kuwapa wosia wa kuwa waadilifu
na kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kufuata misingi na kanuni za skauti.
![]() |
Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini) |
Pia alimalizia kwa kusema kuwa "Jukwaa la vijana ni moja ya chombo kinacho tumiwa katika kufanikisha shughuli za chama, hivyo ni vyema vijana kukitumia chombo hicho katika kuleta mafanikio ndani ya chama..
Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro. |
Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro. |
Vijana wa skaut wakiwa katika kongamano mkoani Morogoro. |
Kamishna mkuu msaidizi Mwl. Merry Anyitike (msimamizi wa programu za vijana nchini)akitoa somo kwa vijana waliohudhuria jukwaa hilo. |
UONGOZI WA KAMATI YA JUKWAA LA VIJANA TANZANIA 2014-2016
![]() |
Bi, ANNA EMMANUEL (Dodoma) NAIBU MWENYEKITI |
![]() |
Ndugu, MURTADHWA RASHID (Dar Es Salaam) KATIBU |
![]() |
Ndugu,TITO JACKSON (DarEs Salaam) MJUMBE |
![]() |
Ndugu, ALLEN MPANDE (Morogor) MJUMBE |
![]() |
Ndugu, ELAM MOSSES (Mbeya ) MTUNZA HAZINA |
Jumamosi, 17 Mei 2014
MESSENGERS OF PEACE.
WAJUMBE WA AMANI {MESSENGERS OF PEACE}
Nimradi ulioundwa na kamati na kamati kuu ya skauti ya dunia kwa kukuza na kuitambua miradi na huduma zinazochangia amani duniani.
*LENGO LA MESSENGERS OF PEACE
- Kuhamasisha mamilioni ya vijana wa kike na wakiume kwa ajili ya dunia kufanya kazi kwa ukaribu na hata kufikia amani.
*NJIA YA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA
-Sanaa
-Vyombo vya habari
-Mitandao ya kijamii
-Mpango wa skauti kutoka makao makuu [wosm] ni kushirikiana na vijana duniani kote juu ya wanayo yafanya na kuhamasisha skauti wenzao dhidi ya kuchukua jitihada hizo katika jamii zao.
*WAENDESHAJI WA MPANGO WA [MOP]
-Mpango mradi huu unaendeshwa na kamati kuu ya skauti duniani [wosm]
-Unasimamiwa na taasisi ya skauti ya dunia pamoja na ..........
-Unatekelezwa na vijana wa kujitolea duniani kote.
*JINSI GANI MRADI HUU UNAVYOENDELEA
-Mpango huu wa [mop] umetokana na miaka 10 iliyopita katika mpango wa "gift of peace" ambao uliongoza [kushiriki nafasi ] kwa zaidi ya skauti millioni 10 katika nchi 110 kwa kufanya kazi ya amani katika jamii [mfano qiblatayn scout group walipata tuzo]
-Mfalme Abdallah [saudi] alibainisha kuwa ni wajumbe wa amani kutokana na mradi huo"Gift of peace"
-Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia skauti duniani aliweka rasmi [Skauti kuwa wajumbe wa amani] sep,2011.
*WADHAMINI WA MRADI
-[WOSM] kama sehemu ya wajumbe wa amani, ofisi ya skauti ya dunia ina mfuko maalum wa kuendesha miradi hiyo duniani kote, kwa mashirika ya skauti katika nchi husika.
*NAFASI YA KUUNGANA NASKAUTI WENGINE
- Unaweza kuweka kupitia miradi waliyofanya skauti wengine duniani kwa kupitia www.scoutmessengers.com
Nimradi ulioundwa na kamati na kamati kuu ya skauti ya dunia kwa kukuza na kuitambua miradi na huduma zinazochangia amani duniani.
*LENGO LA MESSENGERS OF PEACE
- Kuhamasisha mamilioni ya vijana wa kike na wakiume kwa ajili ya dunia kufanya kazi kwa ukaribu na hata kufikia amani.
*NJIA YA KUFANYA KAZI KWA PAMOJA
-Sanaa
-Vyombo vya habari
-Mitandao ya kijamii
-Mpango wa skauti kutoka makao makuu [wosm] ni kushirikiana na vijana duniani kote juu ya wanayo yafanya na kuhamasisha skauti wenzao dhidi ya kuchukua jitihada hizo katika jamii zao.
*WAENDESHAJI WA MPANGO WA [MOP]
-Mpango mradi huu unaendeshwa na kamati kuu ya skauti duniani [wosm]
-Unasimamiwa na taasisi ya skauti ya dunia pamoja na ..........
-Unatekelezwa na vijana wa kujitolea duniani kote.
*JINSI GANI MRADI HUU UNAVYOENDELEA
-Mpango huu wa [mop] umetokana na miaka 10 iliyopita katika mpango wa "gift of peace" ambao uliongoza [kushiriki nafasi ] kwa zaidi ya skauti millioni 10 katika nchi 110 kwa kufanya kazi ya amani katika jamii [mfano qiblatayn scout group walipata tuzo]
-Mfalme Abdallah [saudi] alibainisha kuwa ni wajumbe wa amani kutokana na mradi huo"Gift of peace"
-Mwenyekiti wa kamati ya kusimamia skauti duniani aliweka rasmi [Skauti kuwa wajumbe wa amani] sep,2011.
*WADHAMINI WA MRADI
-[WOSM] kama sehemu ya wajumbe wa amani, ofisi ya skauti ya dunia ina mfuko maalum wa kuendesha miradi hiyo duniani kote, kwa mashirika ya skauti katika nchi husika.
*NAFASI YA KUUNGANA NASKAUTI WENGINE
- Unaweza kuweka kupitia miradi waliyofanya skauti wengine duniani kwa kupitia www.scoutmessengers.com
Jumanne, 4 Februari 2014
SKAUTI WATOA MSAADA WA HUDUMA KATIKA MAAFA YA MAFURIKO MJINI MOROGORO-DUMILA.
SKAUTI WATOA MSAADA WA HUDUMA KATIKA MAAFA YA MAFURIKO MJINI MOROGORO-DUMILA.
Skauiti washiriki katika kutoa msaada
katika maafa ya mafuriko yaliyo tokea mjini morogoro-dumila dhidi ya
mvua zilizo nyesha kwa wingi hadi kupelekea mafuriko wilayani
humo{dumila}. kufuatia maafa hayo chama cha skauti tanzania kupitia
kamishna msaidizi kitengo cha maafa kilipeleka kikosi cha huduma na
uokoaji majini na nchikavu ili kushirikiana na vikosi vyengine vya
serikali na binafsi katika kutoa msaada unaohitajika.
Ni wanachama wapya wa skauti ambao walikubali kwa moyo wa dhati kujiunga na chama cha skauti baada ya kuona yale waliofanya skauti katika kusaidia kijiji chao baada ya mafuriko kutokea.
Kamishna mkuu msaidizi kitengo cha maafa. Alhajj, Juma Massud
Kufuatia tukio hilo skauti pia iliweza kuzaa matunda juu ya jambo kubwa
wlilolifanya katika kambi ya dhalura iliyo tengenezwa kufuatia tukio
hilo, serikali kupitia mkuu wa mkoa wa morogoro iliikabidhi skauti
dhamana ya kuandaa na kuweka maingira ya kambi kwakuwa skauti ni wazoefu
juu ya masuala ya kambi.
Skauti wakiwa katika shughuli za ujenzi wa vyoo kwaajili ya kukamilisha
zoezi la uaandaji wa eneo la kambi kama walivyo agizwa na mkuu wa mkoa
wa morogoro.
Skauti wakiwa katika shughuli za ujenzi wa vyoo kwaajili ya kukamilisha
zoezi la uaandaji wa eneo la kambi kama walivyo agizwa na mkuu wa mkoa
wa morogoro.
Lakini pia kama Skauti walichukua nafasi hiyo kwa kukitan
gaza chama cha Skauti katika jamii na kusambaza ujumbe wa Amani kupitia
vijana wa shule ya sekondari Dumila na wana kijiji kiujumla. pia
waliweza kuanzisha kundi la skauti na kulipa mafunzo ya mwongozo kwa
kuanzia juu ya skauti na shughuli zake kiujumla.Ni wanachama wapya wa skauti ambao walikubali kwa moyo wa dhati kujiunga na chama cha skauti baada ya kuona yale waliofanya skauti katika kusaidia kijiji chao baada ya mafuriko kutokea.
Vijana wadogo wakiwa pamoja na skauti katika kuashiria upendo wa dhati
juu ya walio watendea baada ya maafa yalio wakuta katika kijiji
chao-dumila.
Wana kijiji wakiwa katika picha ya pamoja na skauti baada ya
kuwahubiria uskauti na madhumuni yake na kuwaachia ujumbe wa Amani ili
waweze kuishi vyema kwa kufuata misingi halisi ya kibinaadamu.
Kiongozi wa kikosi chahuduma na uokoaji{majini} akiwa katika kiashirio
cha Ujumbe wa Amani baada ya kuzungumza na wakaazi wa kijiji cha Dumila
mjini Morogoro.
Kiongozi wa kikosi cha maafa na uokoaji{majini}, pia ni msimamizi wa
vijana katika masuala ya Ujumbe Amani Tanzania {katika ngazi ndogo ya
Taifa} akiwa na mmoja kati ya vijana wa kijiji hicho kilicho kumbwa na
maafa ya mafuriko.
Mwisho kiongozi huyo aliwataka skauti wote kuwa naa ushirikiano wa
pamoja katika kukijenga chama cha skauti katika misingi na maadili
yaliyo mema, na kuwa tayari akati wowote kulitumikia taifa pale
inapotokea tatizo kama hilo la mafuriko na mengineyo. pia alisisitiza
juu ya kundi hilo jipya la skauti kuwa na moyo wa upendo kwa kila mmoja
na kpeana ushirikiano na kuishi kutokana na misingi, kanuni na ahadi ya
skauti.
Jumatano, 8 Januari 2014
vijana wa skauti kanda ya afrika mashariki wakijadili kuhusu masuala ya
vijana katika mkutano kuu wa nane wa kanda hiyo ya Afrika Mashariki
huku kaulimbiu ikisema (scout promoting peace and good citizen ship).
waongoza mada wakisikiliza hoja kutoka kwa wajumbe wa wa mkutano huo.(kutokea kulia ni Malik kutoka Tanzani, anaefata ni Benta kutokea Kenya, anefata ni Brian kutokea uganda na wamwisho ni prience kutokea Burundi)
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huowa nane wa kanda ya Afrika mashariki kutokea kulia ni Murtadhwa (Tanzania), Anita (Uganda), Anna(Tanzania) na Khalid (Uganda).
moja ya waongoza mada (Malik) wa kutokea Tanzania alikua akizungumzi juu ya kaulimbiu ya mkutano huo isemayo "skauti kutangaza Amani na kuwafanya raia kuwa wema
waongoza mada wakisikiliza hoja kutoka kwa wajumbe wa wa mkutano huo.(kutokea kulia ni Malik kutoka Tanzani, anaefata ni Benta kutokea Kenya, anefata ni Brian kutokea uganda na wamwisho ni prience kutokea Burundi)
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huowa nane wa kanda ya Afrika mashariki kutokea kulia ni Murtadhwa (Tanzania), Anita (Uganda), Anna(Tanzania) na Khalid (Uganda).
moja ya waongoza mada (Malik) wa kutokea Tanzania alikua akizungumzi juu ya kaulimbiu ya mkutano huo isemayo "skauti kutangaza Amani na kuwafanya raia kuwa wema
No comments:
Post a Comment