Monday, July 28, 2014




MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA DAR ES SALAAM‏



Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akikimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi tayari kuanza ziara yake Mkoani Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (mwenye T-shirt nyeupe) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza akikimbiza mwenge wa Uhuru Tayari kwa kuukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadiki.
(Picha na Hassan Silayo na Benjamin Sawe)

(Yesterday)

GPL

MWENGE WA UHURU WAWASILI MKOA WA DAR ES SALAAM‏


 Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo akikimbiza Mwenge wa Uhuru kwa ajili ya kuukabidhi tayari kuanza ziara yake Mkoani Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo (mwenye T-shirt nyeupe) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bi. Mwantumu Mahiza leo jijini Dar es…

5 days ago

Michuzi

MIRADI IWE ENDELEVU SIYO KWA MWENGE TU - RACHEL KASANDA


VIONGOZI na watendaji mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo inayozinduliwa katika kipindi cha mbio za mwenge iwe endelevu ili iwasaidie wananchi na si kwa ajili ya mbio hizo.
Baadhi ya miradi imeonekana kuzinduliwa na viongozi wa mbio za mwenge lakini baada ya muda inakufa jambo ambalo si malengo ya miradi hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa wananchi katika kutatua changamoto za kupata huduma za kijamii.
Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Kasanda kwenye kijiji cha Bungu wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa stendi ya mabasi ya Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani humo.
Kasanda amesema kuwa miradi hiyo inapaswa kuwa endelevu ili jamii iweze kunufaika na si kuwa ya muda kwa ajili ya mwenge kwani hiyo ni michango ya wananchi, wahisani na serikali hivyo lazima iwe na manufaa.
Amesema kuwa Viongozi wanapaswa kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi baada ya kuzinduliwa kwa kuwa endelevu na kutoa matunda ambayo yanatarajiwa na wananchi kutokana na ujenzi wake.
Amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya miradi hiyo kwa muda tu ambapo ikishazinduliwa inaachwa hapo hapo pasipo kuendelezwa na kusababisha kufa jambo ambalo halipaswi kuendelea kufumbiwa macho.
Aidha viongozi na watendaji ndiyo watu wa kuwaonyesha njia wananchi kwa hivyo wanapaswa kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na mafanikio kwa wananchi ili kuwaondolea changamoto za upatikanaji wa huduma za kijamii.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Nurdin Babu amesema kuwa yeye kama kiongozi kwa kushirikiana na watendaji, viongozi na wananchi watahakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu ili iwe na manufaa kwa wananchi.
Babu amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa kwa walengwa ambao ni wananchi kwani wamekuwa na changamoto nyingi ambazo zinatatuliwa hatua kwa hatua kwa kuwashirikisha wadau wa maendeleo. Mbio hizo za mwenge leo zitakuwa wilaya ya Kibaha.

1 week ago

Michuzi

MAMIA YA WANANCHI SOMANGA KILWA WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE,KAYA 70 ZAJIUNGA NA CHF PAPO KWA PAPO WAKIPOKEA MWENGE WA UHURU


Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2014,Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa kilwa kujiunga na CHF,kwani ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa kuzingatia maboresho ya huduma za afya yanavyowezekana chini ya sera ya urasimishaji wa majukumu kwa jamii hususani ya uchangiaji baina ya wananchi na serikali,ambapo mfuko wa taifa wa bima ya afya unasimamia mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa uhuru.
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya na mwitikio wa wananchi wa kilwa ambapo takribani wananchi 257 walijitokeza kupimwa afya na kaya 73 zilijiunga papo kwa papo na CHF Kwenye banda la mfuko kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye alikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya shule ya msingi somanga ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe. Abdallah Ulega.
Mkazi wa kata ya somanga Fatuma Likondwe akipata huduma ya upimaji wa shinikizo la damu kutoka kwa daktari Salama Bimbire,zaidi ya watu 257 waliweza kupatiwa huduma za vipimo kwa magonjwa yasiyoambukiza na wastani wa asilimia 58% ya waliopimwa walikutwa na shinikizo la damu (BP) na hawakujitambua hapo kabla.Wananchi wa Kilwa wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda la Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha sukari kwenye damu (RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na urefu wa mwili (BMI) na ushauri wa kitaalamu ulitolewa na madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Somanga-Kilwa.Picha na Paul Marenga-NHIF LINDI

1 week ago

Michuzi

WAZIRI CHIKAWE ASHIRIKI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU JIMBONI KWAKE NACHINGWEA LEO


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akipokea Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Chiola, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya Mwenge huo kumaliza kukimbizwa katika Wilaya Ruangwa. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akisalimiana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda baada ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru uliotoka Wilaya ya Ruangwa na kuingia Wilaya ya Nachingwea. Wapili Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo ambaye ndio aliyekabidhiwa rasmi Mwenge huo kutoka Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (kulia) akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Chiola (hawapo pichani) baada ya kufungua Mradi wa Nyumba ya Mganga katika Kijiji hicho kilichopo Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda (aliyebeba ndoo ya maji) akishangiliwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (wapili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Regina Chonjo pamoja na wananchi baada ya kubeba ndoo ya maji baada ya kufungua mradi wa maji katika Kijiji cha Mituguru, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Regina Chonjo. Mwenge wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” umengia katika wilaya hiyo ambapo unatarajiwa kufungua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo. Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ikungu, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi baada ya kukabidhi Bajaj kwa walemavu na Pikipiki kwa watendaji wa Wilaya na Kata mbalimbali katika wilaaya hiyo zikiwa ni kwa shughuli za maendeleo katika Halmashauri hiyo. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe. Mwenge huo wa Uhuru ambao mwaka huu 2014 umebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, Jitokeze Kupiga Kura ya Maoni tupate Katiba mpya” utakimbizwa katika Wilaya ya Nachingwea ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo itafunguliwa pamoja na kuzinduliwa. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto), akiwasalimia wapiga kura wake wa Kijiji cha Ikungu wakati wa ukimbizaji wa Mwenge wa Uhuru katika Jimbo lake la Nachingwea. Waziri Chikawe alimshukuru Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mwaka 2014, Rachel Kassanda pamoja na timu yake kwa kuzindua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake. Picha na zote na Felix Mwagara.

2 weeks ago

Michuzi

SHIWATA KUTOA VIWANJA BURE OFA YA MWENGE MKURANGA


Na Mwandishi Wetu
WILAYA ya Mkuranga imepanga kupeleka Mwenge wa uhuru katika kijiji cha wasanii kilichopo MWANZEGA, Mkuranga Julai 22, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim  Taalib alisema jana kuwa mwenge utapokelewa kutoka wilaya ya Rufiji katika kijiji cha Kiparang?anda na baadaye utakwenda moja kwa moja katika kijiji cha wasanii na wanamichezo cha Mwanzega ambako utawasili saa 7 mchana.
Alisema kutokana na ujio wa ugeni huo mkubwa SHIWATA imetangaza ofa ya  siku kumi ambapo itapokea wanachama kwa punguzo la asilimia 50 na kugawa bure viwanja vya kujenga nyumba wasanii na wanamichezo ambao watapata nafasi ya kwenda katika sherehe na watakabidhiwa viwanja vyao.
Wasanii na wanamichezo zaidi ya 600 wanatarajiwa kuondoka makao makuu ya shiwata ilala bungoni saa 12 asubuhi Jumanne asubuhi kwenda mkuranga.
Katika sherehe hizo kiongozi wa mbio za Mwenge, ataweka jiwe la msingi katika kijiji cha wasanii kuzindua rasmi kijiji hicho ambacho kinatarajiwa kuwekwa umeme, barabara na miundombinu ya kisasa.
Taalib alisema katika sherehe hizo msanii  maarufu wa atavishwa joho ya kutawazwa kuwa balozi wa kwanza wa kijiji cha wasanii na wanamichezo hapa nchini.
SHIWATA pia inatoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuuu wa Wilaya ya Mkuranga, Viongozi wa Tarafa ya Shungubweni kata ya Mbezi,viongozi wa Mwanzega,Ngarambe.
Alisema kutakuwa na mkutano wa wasanii

2 weeks ago

Tanzania Daima

Serikali yaibeba CCM kwa mwenge


LICHA ya mikusanyiko yote ya kisiasa na kidini kuzuiliwa kwa muda katika mikoa ya Lindi na Mtwara, kutokana na hali ya usalama kuwa tete kufuatia vurugu za gesi, serikali imeruhusu...

2 weeks ago

Tanzania Daima

Ufisadi mbio za Mwenge


PAMOJA na Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusisitiza kuwa michango kwa ajili ya mbio za Mwenge wa Uhuru ni hiari na watu wasichangishwe kwa lazima, Tanzania Daima imebaini...

1 month ago

Tanzania Daima

Mwenge wazindua miradi saba ya bil.1/-


MIRADI saba yenye thamani ya sh 1,029,561,685 imezinduliwa na mbio za mwenge wa uhuru wilayani Kilombero, mwaka huu. Akizungumzia hilo mjini hapa jana, Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, Hassan Masala,...

1 month ago

Habarileo

Katibu Chadema, wenzake washiriki mbio za Mwenge


VIONGOZI wa vyama vya upinzani mjini Morogoro, wameshiriki katika Mbio za Mwenge wa Uhuru. Viongozi hao walioshiriki katika mbio hizo ni Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Morogoro, Ngonyani Boniface, Mwenyekiti wa TLP Wilaya ya Morogoro, Juma Kasielo, Mwenyekiti wa Chama cha Jahazi Asilia, Ismail Rashid na Katibu wa UDP Wilaya ya Morogoro, Salum Mwandule.

1 month ago

Uhuru Newspaper

Mwenge kuzindua miradi ya mamilioni wilayani Gairo



NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
MIRADI saba yenye thamani ya sh. milioni 510 inatarajiwa kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi katika mbio za Mwenge wa Uhuru  wilayani Gairo mkoani Morogoro.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Khanifa Karamagi alisema hayo juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema  Mwenge wa Uhuru utapokewa  leo katika mpaka wa Mkoa wa Morogoro na Dodoma ukitokea wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Khanifa alisem  kati ya miradi  itakayozinduliwa katika wilaya hiyo ni nyumba mbili za kuishi watumishi wa mamlaka ya mji mdogo wa Gairo  na nyumba  ya kulala wageni iliyopo katika eneo la Ukwamani  Gairo, zahanati  ya  Kijiji cha Madege na  mradi wa shamba darasa la ufugaji nyuki na hifadhi ya mazingira Kata ya Msingisi.
Kwa upande wa miradi itakayowekewa mawe ya msingi ni  zahanati katika Kijiji cha Kwipipa na  mradi wa uchimbaji kisima cha maji Kata ya Kibedya na ujenzi wa  nyumba ya mwalimu Chakwale.
Mkuu huyo wa wilaya aliwashukuru wananchi kwa kuchangia nguvu na mali zao katika maandalizi hayo  na kuwataka kujitokeza kwa wingi katika mapokezi hayo.

2 months ago

Tanzania Daima

Kiongozi mbio za mwenge awashauri wasomi


WASOMI wa vyuo vikuu nchini wameshauriwa kujiunga kwenye vikundi vya ujasiriamali badala ya kupoteza muda wakitafuta ajira. Ushauri huo ulitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na kiongozi  wa Mbio za Mwenge...

2 months ago

CloudsFM

MWENGE WA UHURU WAPATA AJALI, POLISI WATATU WAJERUHIWA


Askari polisi watatu kati ya watano, wameumia vibaya baada ya gari walilokuwa wakisindikizia Mwenge wa Uhuru kupata ajali mkoani Singida huku waandishi wa habari na wapigapicha wakinyang’anywa vitendea kazi na kiongozi wa Mbio za Mwenge, Rachel Steven.
Kitendo hicho kilielezwa kuwa ni kuwazuia waandishi wa habari kutuma taarifa za ajali hiyo kwenye vyombo vyao vya habari. Mzozo mkali uliibuka kwa waandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), kituo cha Televisheni cha ITV na Redio One na mwandishi wa Redio Standard waliokuwa kwenye msafara huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, (SACP), Geofrey Kamwela alipotafutwa ili aelezee tukio, alisema hana taarifa kamili na kutaka apewe muda ili afutilie suala hilo aeleze ajali hiyo. Hata hivyo baadaye alipotafutwa jioni alipotafutwa alisema kuwa atatolea taarifa suala hilo leo.

Ajali hiyo iliyohusisha magari matatu ilitokea katika Kijiji cha Kirumbi, Wilaya ya Sikonge, mpakani mwa mikoa ya Tabora na Singida ikiwa ni siku ya kwanza ya mbio za Mwenge huo ulioingia mkoani Singida ukitokea Mkoa wa Mbeya.

Mashuhuda wa ajali hiyo, walisema kuwa ilitokea muda mfupi baada ya Mwenge kupokewa katika Kijiji cha Rungwa kilichopo Kata na Tarafa ya Itigi. Ilielezwa kuwa gari moja la polisi lililokuwa kwenye msafara lilipasuka gurudumu na kusimama pembeni mwa barabara.

Gari jingine la polisi lililokuwa kwenye msafara lilisimama ghafla kutaka kufahamu kilichowapata wenzao, ndipo gari la Ofisi ya Afya ya Mkoa likiwa na wahudumu wa afya, lililigonga kwa nyuma gari hilo.

Kwa kuwa kila gari lilikuwa kwenye mwendo wa kasi ili kuendana na gari la Mwenge lililokuwa limetangulia, gari jingine lililokuwa na askari waliokuwa wamening’inia juu nalo lililigonga gari hilo la afya kwa nyuma na kusababisha askari hao kuumia.

Katika tukio hilo, hakuna hata mmoja kati ya wahudumu wa afya aliyeumia, lakini ajali hiyo ilisababisha askari mmoja kuvunjika mguu, mwingine kuvunjika mkono huku wawili hali zao zikiwa nzuri na mwingine alikuwa mahututi.

Baada ya tukio hilo, waliwahishwa kwenye Hospitali ya Misheni ya St. Gasper iliyopo Itigi kwa matibabu zaidi.

>>Mwananchi

2 months ago

Mwananchi

Mwenge wapata ajali, polisi watatu wajeruhiwa


Askari polisi watatu kati ya watano, wameumia vibaya baada ya gari walilokuwa wakisindikizia Mwenge wa Uhuru kupata ajali mkoani Singida huku waandishi wa habari na wapigapicha wakinyang’anywa vitendea kazi na kiongozi wa Mbio za Mwenge, Rachel Steven.

2 months ago

Dewji Blog

Mwenge wa Uhuru kuwasili Singida na kuzindua miradi ya bilioni 5.9


DSC01298
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk, Parseko Kone akizungumza na waandishi wa habari juu ya ujio wa Mwenge wa Uhuru Mkoani Humo.
DSC01290
Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Lianna Hassan akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Singida kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ujio wa Mwenge wa Uhuru.
DSC01291
Wajumbe wa Mwenge akiwemo Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Manyoni Salum Mkuya, na Afisa Michezo Mkoa wa Singida, Henry Kapera.
DSC01296
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Singida wakiwa kwenye kikao.
DSC01297
Wakimbiza mwenge wa Uhuru Kimkoa wa Singida.
DSC01299

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao cha Mkuu wa Mkoa wa Singida wakati wa kupewa taarifa ya  Mwenge.
Na Hillary Shoo, SINGIDA.
JUMLA ya Miradi 60 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5.95 inatarajiwa kutembelewa, kuzinduliwa na kuwekewa mawe ya msingi Mkoani Singida.
Mkuu wa Mkoa huo Dk, Parseko Kone amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake jana kuwa mwenge huo unatarajiwa kuwasili katika kijiji cha Rungwa Wilayani Manyoni leo ukitokea Mkoa wa Mbeya.
Aidha Dk, Kone alisema miradi hiyo ni ya sekta ya elimu, maji, Afya, Barabara, Biashara, Mazingira , Kilimo, Mifugo, Ushirika, misitu na sekta binafsi.
“Ndugu wananchi wa Mkoa wa Singida naitoe wito kwenu mjitokeze kwa wingi katika maeneo yote ambayo mwenge wa Uhuru utapita yakiwemo maeneo ya mapaokezi na kukabidhi, pia Mwenge wa uhuru uwe ni sababu ya kuendelea kuhimiza maendeleo kwenye maeneo yetu kupitia miradi itakayowekewa mawe ya msingi, kuzinduliwa na kufunguliwa.” Alisisitiza Kone.
Aidha aliwataka wananchi kuisimamia miradi itakayowekewa mawe na msingi ili thamani halisi ya fedha zitakazotumika iweze kupatikana na kuikamilisha kwa wakati.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa aliwahimiza wananchi kuzipokea salamu za wakimbiza mwenge wa uhuru Kitaifa, kuzingatia ujumbe utakaotolewa hasa suala la kukamilisha mchakato wa uundaji wa Katiba ambayo ni sheria kuu ya nchi.


NHC YAMWAGA MASHINE 640 ZA KUFYATULIA MATOFALI KWA WILAYA 160

SHIRIKA LA NYUMBA NHC LAENDELEA KUONGEZA AJIRA KWA VIJANA

1  
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Rachel Kassanda akikabidhi mashine nne kati ya  640 zenye thamani ya sh. mil. 288.za kufyatulia matofali kwa Hassan Soud Katibu wa kikundi cha Changamoto kwa niaba ya vikundi vingine vya wilaya ya Ilala ambazo zimetolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), wakati wa mkesha Ilala Bungoni, Dar es Salaam jana. Mashine hizo zilikabidhiwa kwa Kassanda na Meneja wa NHC Kanda ya Ilala, Jackson Maagi (kushoto). Mashine 640 zitagawiwa katika halmashauri za wilaya 160 nchini.
3
Askari wa Kikosi cha FFU wakiulinda mwenge mara baada ya kuwasili Ilala Boma mahali ambapo ndiyo kituo ulipolala mwenge huo.
4
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Kanda ya Ilala, Jackson Maagi wa pili kutoka kushoto akiwa pamoja na wafanyakazi wnzake kabla ya kukabidhi mashinne hizo jana.
2
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC Bw. Jackson Maagi akizungumza wakati wa kukabidhi mashine hizo jana
………………………………………………………………………………..
HOTUBA FUPI YA MENEJA WA NHC ILALA KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA
Ndugu kiongozi wa Mbio za mwenge,
Ninayo furaha kubwa sana kusimama mbele yenu na kuongea nanyi kama mwakilishi kutoka Shirika la Nyumba la Taifa.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge; Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango mkakati wake wa miaka mitano ambao moja ya malengo yake sita makuu ni kuboresha taswira ya Shirika.
Katika utekelezaji wa lengo hili, Shirika lina sera ya huduma kwa jamii ambayo imejikita katika kusaidia vijana kujiajiri. Ili kuwezesha vijana kujiajiri, Shirika limeamua kuzisaidia Halmashauri za Miji na Wilaya kote nchini mashine za kuwezesha vikundi vya vijana kutengeneza matofali ya kujengea nyumba. Nchi yetu ina Halmashauri 160 na kila Halmashauri itapewa mashine 4 kwa ajili ya kusaidia vikundi vya vijana. Katika mpango huu jumla ya mashine 640 zitatolewa na Shirika na kugharimu shilingi 288,000,000/.
Aidha, kila Halmashauri itapatiwa shilingi laki tano (500,000/=) kama mtaji kwa vijana kuanzia shughuli yao ya kutengeneza matofali. Kadhalika, Shirika limegharamia shilingi 800,000/= kwa kila Halmashauri kwa ajili ya kuwalipa wakufunzi kutoka VETA wanaotoa maelekezo kwa vijana namna ya kutumia mashine hizo.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge,katika kutekeleza mradi huu jumla ya shilingi milioni mia saba (700,000,000/=) zitatumika. Aidha, tunatarajia kuwa ajira zaidi ya 8,000 za moja kwa moja na ajira nyingine zaidi ya 200,000 zisizo za moja kwa moja zitapatikana.
Katika mpango huu kila Wilaya inatakiwa kuwa na vijana 40 watakaokuwa katika vikundi vya watu 10 kila kimoja. Msaada huu ni mkubwa lakini kutokana na ukubwa wa tatizo la ajira jitihada zaidi kutoka kwa wadau mbalimbali zinatakiwa. Ni matarajio yetu kuwa taasisi nyingine ama mtu mmoja mmoja atashiriki kukwamua vijana hawa.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, kupitia maadhimisho haya, Shirika linatoa mashine nne (4) kwa vikundi 4 vya vijana vilivyoundwa katika wilaya ya Ilala ambapo kila kikundi kina jumla ya vijana10 watakaotumia mashine moja. Hivyo jumla ya vijana 40 katika Wilaya hii watapata ajira kutokana na mashine hizi.
Ndugu Kiongozi wa Mbio za Mwenge, mwisho Shirika linatoa rai kwa Taasisi za serikali, mashirika ya umma, binafsi na watu mbalimbali, kuunga mkono juhudi za Serikali za kupunguza tatizo la ajira kwa vijana. Ni matumaini yetu kuwa tutawaunga mkono kwa kununua matofali yao ama kusaidia upatikanaji wa mashine nyingine zaidi ili wengine ambao hawajafikiwa na mradi huu wafikiwe na wapate kufaidika.
Kipekee tunaomba Serikali za Mitaa (kwa maana ya Halmashauri zetu za wilaya, miji, manispaa ama jiji) wawe ni wanunuzi wakuu wa matofali yatakayotengenezwa na vikundi hivi vya vijana ambayo ni ya gharama nafuu ili kusaidia miradi mbalimbali ya ujenzi na kuwaongezea kipato chao. Tunawaomba pia msaidie kusimamia mradi huu ili uweze kuwa endelevu.