Showing posts with label HOME. Show all posts
Showing posts with label HOME. Show all posts

Thursday, November 13, 2014

Taarifa. Taarifa. Taarifa.

Kwa jasiri skauti (Rover's scout) wote tuna waalika kushiriki jukwaa la vijana la kanda ya Afrika Mashariki litakalo fanyika huko Kigali, nchini Rwanda,kuanzia 27 Nov hadi 31 Nov kwa maelezo na watakao kuwa tayari kushiriki tafadhali wasiliana na Mwenyekiti au Katibu mkuu wa Jukwaa la vijana Tanzania.

Wednesday, November 12, 2014

WATU WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA BASI LA WIBONELA KUPINDUKA MJINI KAHAMA LEO





 Basi la Wibonela linalofanya safari zake kahama Dar limeua watu zaidi ya watano na kujeruhi wengi leo asubuhi eneo la Fantom Kahama. Chanzo ni mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kukata kona ya kuingia barabara kuu hivyo kuruka nje na kusababisha basi hilo kupinduka. Na pia kibaka aliyekuwa anapekua na kuchomoa fedha na Vitu kwa majeruhi wa ajali hiyo amepigwa na kuchomwa moto hadi kufikia na watu wenye hasira kali. Mpaka sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni wangapi.

Monday, October 13, 2014

Mwenge wa Uhuru

SKAUTI WILAYA YA ILALA WASHIRIKI KUUPOKEA MWENGE WA UHURU
Skauti wilaya ya Ilala wakiwa pamoja na wakimbiza Mwenge katika mapokezi ya Mwenge wa Uhuru kutoka wilaya ya Temeke kwenda wilaya ya Ilala tarehe 26/06/2012 eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Skauti wilaya ya Iala wakiwavisha skafu wakimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa katika viwanja vya Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.
 Mkuu wa wilaya ya Temeke Mh. Sophia Mjema akimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Raymond Mushi tarehe 26/06/2012 katika eneo la Stesheni ya TaZara, Dar Es Salaam.


SKAUTI WILAYA YA ILALA WAENDESHA MAFUNZO YA UONGOZI WA KIKOSI  
PATROL LEADER COURSE- (PEER EDUCATOR TRAINING)
Wahitimu wa mafunzo ya uongozi wa kikosi wilaya ya Ilala wakionyesha vyeti vyao baada ya kuhitimu mafunzo hayo katika viwanja vya makao makuu ya Skauti Dar Es Salaam. Mafunzo hayo yalianza tarehe 22/06/2012 mpaka 24/06/2012.
Kamishina wa Skauti Mkoa wa Dar-Es-Salaam Abubakar Mtitu (aliyevaa fulana ya mistari) akiwapa maelekezo ya mchezo wa kuonyesha umuhimu wa kutunza kumbukumbu washiriki wa mafunzo hayo.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakisikiliza jambo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakiwa katika hema wakibadilishana mawazo juu ya mafunzo ya uongozi wa kikosi
 Scouts Life Saving Activity
 
Sherehe ya kuapishwa kwa Skauti Mkuu Kanali mstaafu .O. Kipingu Ikulu jijini Dar es Salaam, mwaka 2008.
Mlezi  wa Skauti Tanzania Mhe. Dkt Jakaya .M. Kikwete (Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (aliyevaa suti nyeusi). Wa kwanza kulia ni Makamo wa Rais Tanzania Mhe. Ali .M. Shein, [kulia kwa rais ni mkufunzi wa Chama cha Skauti Tanzania ndugu Ngunga.


Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Mwantumu Mahiza aliyevaa kofia ya kijani akibadilishana mawazo na wajumbe wa mkutano wa Skauti wa nchi za Afrika Mashariki mjini Morogoro katika kambi ya Bahati, mwaka 2008.