![](https://scontent-b.xx.fbcdn.net/hphotos-xfp1/v/t1.0-9/s480x480/1376655_1072770006070750_8855280116682557099_n.jpg?oh=427cd0affe0eff2be587fdc9427d390d&oe=54E6538A)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete alfajiri ya jana, Jumamosi, Novemba 8, 2014, alifanyiwa upasuaji
wa tezi dume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko
Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.
Rais Kikwete amefanyiwa
upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake
kujiridhisha kuwa Rais alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.
Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua kiasi cha saa moja
unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa.
Hali ya MheshimiwaRais Kikwete inaendelea vizuri, bado yuko wodini
akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.