Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni sawa na ndoa ya mkeka’
Posted Jumapili,Decemba9 2012 saa 10:20 AM
Posted Jumapili,Decemba9 2012 saa 10:20 AM
Kwa ufupi
“Hakujawahi kuwepo kwa nchi inayoitwa Tanzania Bara
wala Tanzania Visiwani. Haya ni mapungufu ambayo Katiba Mpya inatakiwa
kuyarekebisha ili historia ibaki kama ilivyokuwa. Tanganyika itambulike
kwa kuwa Muungano uliopo ni kati ya nchi ya Tanganyika na nchi ya
Zanzibar,” anasema Adventina Ndibalema mkazi wa Kimara Korogwe.
MCHAKATO wa utoaji wa maoni ya Katiba Mpya
unaendelea kwenye mikoa sita katika awamu hii ya nne. Mikoa ambayo Tume
iko katika kuchukua maoni ya wananchi ni Arusha, Dar es Salaam, Mara,
Simiyu, Geita pamoja na Zanzibar Mjini Magharibi. Katika mikutano hiyo
ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wananchi wamekuwa wakitoa maoni mengi
yenye hoja tofauti.
Katika mikutano hiyo, wajumbe wa Tume wamekuwa
wakiwahimiza wananchi kushiriki kwa uhuru katika kutoa maoni yao bila
hofu. Wito huo wa Tume umekuwa ni jambo la msingi ikizingatiwa kwamba
Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kuogopa na hata kukosa ujasiri wa
kuzungumza hadharani kwa kuikosoa ama Serikali au viongozi wake kwa
hofu ya kuogopa kukamatwa au kufuatiliwa na vyombo vya usalama.
Katika mchakato unaoendelea wa ukusanyaji wa maoni
ya wananchi, imeshuhudiwa wananchi hao wakijieleza kwa uhuru bila hofu
kwenye mikutano mbalimbali ya Tume.
Hii ni haki yao ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hii ni haki yao ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kitu ambacho wananchi kwenye kila mkutano wa Tume wamekizungumzia ni suala la Muungano wa Serikali tatu.
Wananchi wengi wamekuwa wakisisitiza kuwa Katiba
Mpya haina budi kuitambua na kuirejesha Serikali ya Tanganyika. Wananchi
hao wamesema kuwa Serikali ya Tanganyika ni haki ya Watanganyika kama
ilivyo kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
“Watanganyika tumekosa fursa ya kuwa na Serikali
tofauti na wenzetu Wazinzibari ambao wao wanayo Serikali. Kwa hiyo
nataka kuona kuwa Katiba Mpya inairejesha Serikali ya Tanganyika ili
kuleta uwiano sawa kati ya pande mbili za Muungano,” anasema Haji Juma
mkazi wa Kata ya Jangwani Jijini Dar es Salaam.
Hoja hiyo inaungwa mkono na Thadeus Mangia mkazi
wa Tabata Kimanga ambaye ameufananisha muundo wa Muungano uliopo kuwa
sawa na ndoa ya mkeka. Anasema kuwa Katiba Mpya inapaswa kuheshimu
uamuzi wa wananchi juu ya aina gani ya Muungano wanaoutaka na siyo
kulazimishwa waishi kwenye Muungano wasioutaka. Mangia anasema kuwa
muundo unaowafaa Watanzania kwa sasa ni Muungano wa Serikali tatu.
Mangia anasema kuwa Muungano wa Serikali tatu
utaondoa manung’uniko yaliyopo miongoni mwa wananchi kuwa upande fulani
unaonewa na upande fulani wa Muungano ndiyo unaofaidika.
Anasema suluhu ya matatizo ya Muungano ni
kuirejesha Serikali ya Tanganyika kama ilivyo kwa Serikali ya Zanzibar
kisha iundwe Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Wananchi hao wanasisitiza kuwa katika Muungano huo
walioathirika ni Watanganyika kwa kupoteza Serikali yao. Wanasema
Wazanzibari wana Rais na Serikali tangu mwanzo wa Muungano, lakini
Watanganyika wamepoteza vyote, yaani Rais na Serikali. Kutokana na hali
hiyo, Mwalimu Florah Ishengoma (50) kutoka Tabata Kimanga anasema kuwa
Muungano uwe wa Serikali moja na hilo likishindikana basi Serikali ziwe
tatu ili na Watanganyika nao wapate haki yao.
“Kila siku wenzetu Wazanzibari wanalalamika kuwa
wao wamemezwa na muundo wa Muungano huu. Sasa ili kuondoa malalamiko,
napendekeza kuwapo Serikali tatu, yaani ya Serikali ya Tanganyika,
Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Kama hilo
haliwezekani napendekeza tuwe na Serikali moja, Rais mmoja na mawaziri
wakuu wawili, mmoja wa Zanzibar na mwingine wa Tanganyika, na hao
mawaziri wakuu wachaguliwe na Bunge,” anasema Hamad Tao mkazi wa Kata ya
Ilala.
Wananchi hao wamezidi kusisitiza kuwa Katiba
iliyopo ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 inapotosha
historia kuhusu suala la Muungano kwa kuwa imeiua Tanganyika na badala
yake imeanzisha kitu kinachoitwa Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.
Wanasema kuwa hakuna nchi inayoitwa Tanzania Bara iliyoungana na
Tanzania Visiwani ikatokea Tanzania.
- Mtoto afichwa kwenye boksi miaka minne
- Mama Zitto alazwa ICU Dar
- Mwandishi jela baada ya aliyemdhamini kutoroka
- Wapinzani wawalaani Lukuvi, Wassira
- Gharama za maisha zapaa Samunge
- Familia yamwachia Mungu kifo cha Meneja Ewura
- Unafuu usitupeleke kwenye bidhaa bandia
- Kweleakwelea ni janga, inafaa washughulikiwe ipasavyo
- Ukarabati Uwanja wa Ndege waila bajeti
- Washauri kutafutwa vyanzo vipya vya fedha
No comments:
Post a Comment