pamoja na mjadala mzito kuhusu muundo wa serikali mbili au tatu,lazima tudumishe muungano tulioachiwa na waasisi wetu, pia wanasiasa muache kufua majina ya waasisi wetu kwa maslahi yenu ya kutaka kujionesha kwa watanzania, sisi watanzania tunawaheshimu sana waasisi wetu na tumechukia sana kudhalilishwa kwao na watanzania wenzetu hasa wanaotuwakilisha kwa mambo makubwa ya kimataifa, hamuoni hata mataifa mengine wanawaenzi hawa waasisi wetu? chukua mfano siku ya mazishi ya marehemu Tata Madiba (Mandela) jina la baba wa taifa letu lilikuwa likitajwa na kuheshimiwa, je ninyi kwanini mmetugeuka? Wanasiasa na vyama venu mjiangalie na mjitathimini kama watanzania wanawakubali kwa matendo yenu mabaya kwa wataifa.