WATU WATANO WADAIWA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA KUFUATIA AJALI YA BASI LA WIBONELA KUPINDUKA MJINI KAHAMA LEO
Basi
la Wibonela linalofanya safari zake kahama Dar limeua watu zaidi ya
watano na kujeruhi wengi leo asubuhi eneo la Fantom Kahama. Chanzo ni
mwendo kasi uliomshinda dereva wa basi hilo kukata kona ya kuingia
barabara kuu hivyo kuruka nje na kusababisha basi hilo kupinduka. Na
pia kibaka aliyekuwa anapekua na kuchomoa fedha na Vitu kwa majeruhi wa
ajali hiyo amepigwa na kuchomwa moto hadi kufikia na watu wenye hasira
kali. Mpaka sasa haijajulikana majeruhi ni wangapi na waliokufa ni
wangapi.
No comments:
Post a Comment