Friday, June 20, 2014
Sunday, February 23, 2014
SKAUTI YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MINNE 2014-2017 NA KUMKUMBUKA MWANZILISHI WA CHAMA HICHO DUNIANI BADEN POWELL
![]() |
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah. |
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Konsolata Mgimba (katikati), ambaye alikuwa mgeni
rasmi katika sherehe hiyo, akikata utepe kuashiria kuzindua mpango
mkakati wa Skauti wa miaka minne 2014-2017 Dar es Salaam jana. Kulia ni
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa
Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah na Makamu Mwenyekiti Skauti Taifa,
Salim Mwaking'inda.
Vijana wa Skauti wakiwa katika kambi
ya mfano katika Maonesho hayo yaliyofanyika Uwanja wa Maonesho ya
Biashara wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa.
Vijana wa Skauti wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Kamishna Mtendaji wa Skauti,
Brigedia General, Gerald Mkude (kushoto), akisaidia kufungua taarifa ya
mpango mkakati wa miaka minne wa Skauti wa 2014-2017. Wengine kutoka
kulia ni Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, ambaye pia ni
Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah, Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Konsolata Mgimba na Makamu
Mwenyekiti Skauti Taifa, Salim Mwaking'inda.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Konsolata Mgimba (katikati), akionesha taarifa ya
mpango mkakati wa miaka minne ya Skauti baada ya kuuzindua rasmi.
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti
Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah
(kulia), akitoa nasaha zake kwa ufupi katika maadhimisho hayo kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi.
Vijana wa Skauti wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti
Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah
(kulia),akimpatia nyenzo za kazi Elibariki Mmari kuwa Kamishna wa Mkoa
wa Mwanza baada ya kumuapisha katika hafla hiyo. Baadhi ya Makamishna wa
Mikoa na Manaibu wao walioteuliwa kushika nafasi hizo waliapishwa.
Baadhi ya Makamishna walioteuliwa kuongoza katika mikoa mbalimbali wakiwa katika hafla hiyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Konsolata Mgimba (kushoto), akimpongeza Kamishna
Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mafia,
Abdulkarim Esmail Hassan Shah kwa kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya
Utendaji na Mweka Hazina wa Shirikisho la Wabunge wa Skauti Duniani.
Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti
Tanzania, ambaye pia ni Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Esmail Hassan Shah
(kulia), akipeana mkono na Kamishna Mteule wa Mkoa wa Arusha, Shakir
Badruddin baada ya kumuapisha katika sherehe hiyo.
Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Konsolata Mgimba (katikati),
akipata maelekezo katika kambi ya mfano ya skauti katika hafla
hiyo.(Imeandaliwa na www.mwaibale.blogspot.comNdege aliyoizindua Nyalandu mbovu
*Ni zawadi ya Ujerumani kwa ajili ya kupambana na ujangili
*Yadaiwa ipo JNIA kwa miaka mitatu, imepakwa rangi juzi tu
*Haijawahi kuruka tangu itue Dar es Salaam kutoka ughaibuni
NA MWANDISHI WETU, Dar
WAKATI
dunia ikiwa katika vita ya kupambana na ujangili, juzi usiku, Waziri wa
Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alizindua ndege iliyotolewa na
Ujerumani kwa ajili ya mapambano hayo.
Ndege
hiyo ilizinduliwa mwishoni mwa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ujerumani Frank-Walter Steinmeier, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Hata
hivyo, taarifa zilizolifikia gazeti hili kutoka kwa vyanzo vyake vya
uhakika zimeweka wazi kuwa ndege hiyo inayotarajiwa kutumiwa na Wizara
ya Maliasili na Utalii kupambana na ujangili, ni mbovu.
Sherehe za uzinduzi huo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali, watendaji wa wizara husika na waandishi wa habari.
“Ndege
hii (iliyozinduliwa), ipo hapa hapa uwanjani (JNIA) kwa kama miaka
mitatu hivi; haijawahi kuruka tangu ifike hapa, sasa iweje leo
ikabidhiwe kwa serikali kupambana na ujangili? Hapa kuna kitu hakijakaa
vyema,” alisema mtoa habari wetu, Ofisa wa Uwanja wa Ndege ambaye ni
wazi hatutoweza kuandika jina lake gazetini kwa sasa.
Alisema
kilichofanyika kabla ya kuzinduliwa kwa ndege hiyo hapo juzi, ni kupaka
rangi iweze kuonekana kama mpya, au walau inaweza kufanya kazi, wakati
ukweli wa ndege hiyo unajulikana.
“Kazi
inayotarajiwa kwenda kufanywa na ndege hiyo ni kubwa kuliko uwezo wake.
Ikitumika, kuna uwezekano mkubwa wa maafa kutokea na Watanzania wenzetu
kupoteza maisha.
“Huu
sasa ni kuuanika umasikini wa nchi yetu hata pasipo na sababu. Ndege
hii haijawahi kufanya safari yoyote kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Kwanini maliasili wakubali kupokea ‘kimeo’,” alisema na kuhoji ofisa
mwingine uwanjani hapo.
Akizungumza
na Raia Tanzania jana, mwanachi mmoja aliishangaa Serikali kushindwa
kununua ndege rasmi kwa ajili ya kupambana na majangili, kama kweli
inahitajika, badala ya kupokea ndege iliyotelekezwa uwanjani kwa miaka
miwili au mitatu.
“Umasikini
ni kitu kibaya sana, unaweza kupewa msaada bandia huku unashangilia.
Kwa nini wizara isitumie wataalamu wa masuala ya ndege waliopo nchini
kuikagua kabla ya kuzinduliwa?,” alihoji.
Hata
hivyo, pamoja na unyeti wa suala hili, bado Waziri wa Maliasili na
Utalii, Nyalandu na katibu mkuu wake, Maimuna Tarishi, hawakutoa
ushirikiano kwa mwandishi wa habari hii.
Nyalandu,
alipopigiwa simu ya mkononi kwa mara ya kwanza saa 6.49 mchana,
hakupokea simu; na alipoandikiwa ujumbe mfupi wa maandishi dakika chache
baadaye, alijibu kwa kifupi ‘I am in a meeting’.
Na alipotafutwa tena saa 8.29 mchana, bado hakupokea na kutuma ujumbe wenye maneno yale yale, kwamba yuko kwenye mkutano.
Wadadisi
wa mambo jijini Dar es Salaam, wamekuwa wakihoji uhalali wa kutumia
nguvu nyingi kupambana na majangili ambao serikali imeshaitangazia dunia
kuwa inawafahamu, na kwamba kinara wao anaishi Arusha.
Mmoja
kati yao, aliliambia Raia Tanzania kuwa ni ajabu kwa serikali kupokea
zawadi za magari na ndege kwa ajili ya kupambana na majangili
wanaofahamika.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal ametoa wito kwa wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kufanya maamuzi yanayozingatia maslahi mapana ya taifa ili kufanikisha upatikanaji wa Katiba itakayokidhi matakwa na matarajio ya wananchi.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kupiga kura ya maoni ili kufanikisha upatikanaji wa katiba shirikishi itakayoliongoza taifa kwa kipindi kirefu bila kuhitaji kufanyiwa marekebisho.
Akizindua Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2014 jana katika uwanja wa Kaitaba, manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Dkt. Bilal amesema mchakato unaoendelea wa upatikanaji wa katiba mpya ni jukumu la watanzania wote na kuongeza kuwa kila mwananchi analo jukumu la kuelewa mchango, wajibu na nafasi aliyonayo ili kukamilisha mchakato huu muhimu.
“Bunge Maalum la Katiba linaendelea na kazi kubwa, nachukua fursa hii kulipongeza kwa hatua linayoendelea nayo naamini maamuzi yote yatakayofikiwa yatazingatia maslahi mapana ya nchi yetu na kutoka na katiba inayokidhi matakwa ya wananchi” Amesema.
Amesema mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu zinabeba ujumbe muhimu usemao Katiba ni Sheria Kuu ya nchi chini ya Kauli inayowahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya maoni ili kuliwezesha taifa kuwa na Katiba mpya.
Dkt. Bilal ameeleza kuwa kila mwaka nchini mbio za Mwenge wa Uhuru huambatana na kauli ya kudumu kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Rushwa , Dawa za kulevya na Malaria kwa lengo la kuwakumbusha wananchi kuendelea kupambana na chanagamoto hizo na kutafuta mbinu za kujikwamua .
Kuhusu changamoto hizo hususan ugonjwa wa Malaria amefafanua kuwa ni kati ya magonjwa yanayosababisha vifo kwa kiwango kikubwa hasa kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 na kuongeza kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huo sharti yapewe kipaumbele katika mbio za Mwenge kwa viongozi wa mbio hizo pamoja na mambo mengine kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa huo katika maeneo yote watakayopita kuanzia mwaka huu na kuendelea.
Ameeleza kuwa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) kuhusu ugonjwa huo zinaonesha kwamba kati ya watu bilioni 3.3 sawa na nusu ya idadi ya watu duniani wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.
Amesema Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi za Bara la Afrika ambazo ugonjwa wa malaria ni moja ya magonjwa yanaoongoza kwa kusababisha vifo kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 na wajawazito imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kukabilia na tatizo hilo.
“Kwa upande wetu serikali tunaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuifanya Tanzania bila Malaria iwezekane kwa wataalam wetu kuendelea kutoa ushauri na maelekezo kwa wananchi, kuimarisha upatikanaji wa dawa na huduma za matibabu katika hospitali zetu,kuhimiza matumizi ya vyandarua vyenye dawa, kuhimiza matumizi sahihi ya dawa za kuzuia malaria kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 5”
Kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini Dkt. Bilal ameeleza kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na jumuiya za kimataifa ili kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya VVU yanapungua na kufikia sifuri ifikapo mwaka 2015.
Akizungumzia mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya nchini amefafanua kuwa jukumu hilo linahitaji juhudi za pamoja kati ya serikali na wananchi na kueleza kuwa kwa upande wa serikali, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya inaendelea kutekeleza jukumu lake ili kuhakikisha Tanzania inakuwa salama.
“Tunatambua kuwa vita ya dawa za kulevye ni kubwa na inahitaji mchango wa kila mwananchi sote tunatakiwa kuungana na tume ili kuisaidia kutimiza majukumu yake”
Kwa upande wake waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akizungumza kabla ya uzinduzi wa mbio hizo amesema kuwa Mbio za Mwenge wa Uhuru zimekuwa zikiwahamasisha wananchi kuibua, kubuni na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo wanayoishi.
Amesema kwa mwaka huu Mwenge wa Uhuru utakimbizwa kwa muda wa siku 165 katika Halmashauri za wilaya zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na zitahitimishwa mwezi Oktoba mwaka huu mkoani Tabora.
Kuhusu ujumbe wa mbio za Mwenge mwaka huu Dkt. Mukangara ameeleza kuwa unalenga kuwahamasisha wananchi popote walipo kushiriki kikamilifu katika mchakato wa katiba mpya ili kupata katiba bora kwa maslahi na mustakabali wa Taifa.
“Kwa kuwa katiba ndiyo sheria kuu ya nchi ni muhimu tukahakikisha kuwa kila mwananchi anatimiza wajibu wake wa kutoa uamuzi wa mwisho kwa njia ya kupiga kura ,nawahakikishia mbio za mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zitafanya kazi hiyo ya kuwahamasisha wananchi kutimiza haki yao kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba ya mwaka 2011 ”
Naye Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe awali akizungumza wakati wa kuwakaribisha viongozi mbalimbali wa serikali, mabalozi, nchi washirika wa maendeleo na viongozi majirani wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru mkoani Kagera zitaweka msisitizo mkubwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, Rushwa,Mapambano dhidi ya madawa ya kulevya, uvunjifu wa amani na kila aina ya chuki na uhasama.
Amesema Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chachu ya maendeleo ya taifa la Tanzania na kufafanua kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka huu ni za kipekee kutokana na umuhimu wake katika mkoa wa Kagera.
“Mwenge wa Uhuru ni chachu kubwa ya maendeleo utaleta matumaini, amani na heshima pale palipojaa dharalau na kwa hakika Mwenge huu utamulika na kuwafichua majambazi wenye silaha, wanaoishi nchini bila kufuata sheria, wezi wa mifugo, wanyanyasaji wa kijinsia, washirikina, waharibifu wa mazingira, wanaojichulia sheria mkononi, wavivu na walevi saa za kazi na wale wenye kuchochea migogoro ya dini na kabila” Amesisitiza.
Ameeleza kuwa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa kwa mwaka 2014 mkoani Kagera zitazindua utekeelezaji wa jumla ya miradi 69 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 69.
Amesema Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika wilaya 7 za mkoa huo ambazo ni Biharamulo, Bukoba, Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Ngara kabla ya kukabidhiwa kwa viongozi wa mkoa wa Kigoma.
Dewji Blog
Vichwa vya Habari Zaidi
Tuesday, June 17, 2014
MWENGE WA UHURU 2014 WAMALIZA MBIO ZAKE MKOANI RUKWA LEO, WAMMULIKA MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) ALIYEKATWA MKONO MWAKA JANA
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya (katikati) akishiriki mbio za Mwenge wa Uhuru (2014) na viongozi wa mbio hizo kitaifa, viongozi na wafanyakazi wa Serikali, vyama vya siasa Mkoani Rukwa na wananchi muda mfupi kabla ya kukabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Abass Kandoro baada ya Mwenge huo kukamilisha mbio zake Mkoani Rukwa leo tarehe 25-05-2014. Mwenge huo wa Uhuru mkoani Rukwa ulitembelea miradi ya maendeleo 28 na vikundi 27 vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni nne (4).
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjCckVLYQS8z1z2vUXzTBad4Hxdkkb4bMAwLWh_oOTNXqdRSpBZxRFI-cDxel0yfC_ZrLKkjjxMs_S0YtTtnr46oEkAX20Hp-uk9N3kJeNb_syFzJbJTo2W3wDTi9__UOQKgeh4jLbmKg8l/s1600/PIC+6.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEh6K8DoMYfPNRvd9I0WT9LHaIdxIIMi3LXMPBfIA40j0wC_lgEBnuSdDwOEl4kRpdsGRUhsqeZUxxW4kHtsK-CQQt1YgNZC9eKKeOUP2mZNpKGcxxIYcVUbi0EE09bvrMsFr9m8gKz0wv5y/s1600/PIC+3.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhJs4fDsDnemgRRJS41NcArnE0N3dUlbyOdCnNztNLG_7mfPzl_BPOSINY4HV7381bP0xbP5B4p2pmUXZhrqMVrEP5h4AUmaKWg5hyphenhyphenrd6iPkIFNo15LcN6EF4CZWju6tuhhMuwBY5BuQ1Gb/s1600/IMG_1859.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijZxIa-3APD5hUVf8ZbLNuxxtmeiThCjnyWdza-5ucbRMHRwLg2_z1KY_z7v1LS6bhjrvv6zhh1N2pzqlPIZN5rV5PYBqpQ7U_cAMXuM96Z3Edqaodpf9D3K1PrHWK7DqUU6ftPZS_WYUh/s1600/PIC+4.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjEuzfXF6hoEs3MaJoydNeSOJhuroz3WLkNDRPNyt3jlx68VJYJQp2WSIFsmOeu23U26YsmdVcHJkTAmZX0ag95m_lpWHQH4iDFoyntii6OMOg5-GoXt1Ys9dWqRJQAqX5UlFc5i9TWy8TL/s1600/PIC+5.jpg)
Mlemavu wa ngozi
Bi. Maria Chambanenge mkazi wa Sumbawanga ambaye alisababishiwa ulemavu
mwingine wa viungo mwaka jana 2013 na watu wasiojulikana baada ya kukatwa mkono
wake wa kushoto kwa imani za kishirikina akishika Mwenge wa Uhuru jana tarehe
24-05-2014 ulipotembelea kijijini kwao kuzindua mradi wa maji na kumkabidhi
msaada wa ng'ombe wawili wa kulimia aina ya Maksai (hawapo pichani) na jembe la
kulimia wanyama (Plau) vikiwa na thamani ya Tsh. Milioni 2.3 kama msaada wa
kujikimu kutoka kwa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kwa mama huyo.
(Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)
Subscribe to:
Posts (Atom)