Wednesday, April 16, 2014

Saturday, April 12, 2014

TAZAMA PICHA 100 ZA MADHARA YA MVUA JIJINI DAR



Kariakoo Jijini Dar hali ya mvua ipo hivi... ni hatari tupu
Foleni nayo usiombeeeeeeeeeeee....

 Sehemu ya maduka yaliyopo eneo la Kituo cha daladala cha ITV yakiwa yamezingirwa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam. Kutokana na mvua hizo na maji kujaa kumesababisha msongamano mkubwa wa mago kuanzia jana jioni na leo.
 Barabara ya kuelekea Goba....
 Barabara ya Goba ikiwa imeharibika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
 Maji yakitiririka kwa kasi katika Mto Mbezi eneo la Bondeni...
 Vijana wakitumia fursa vizuri kwa kujipatia mchanga unaotiririshwa na maji ambapo huwauzia madereva wa maroli.
 Eneo la Mwenge karibu na kituo cha daladala.....
 Moja ya daladala lililokuwa gereji likiwa limezingirwa na maji eneo la Mwenge....
 Maduka ya Mwenge yakiwa yamezingrwa na maji.....
 Mdada huyu alikuwa akipiga hesabu na kujiuliza jinsi ya kuvuka maji yaliyojaa na kukatiza barabara eneo la ITV.
 Mwenge karibu na Zahanati...... hakuna njia ya kuingilia Zahanati
 Maduka eneo la Mwenge yamejaa maji....
 Kazi haifanyiki leo katika maduka haya...
 Mwenge eneo la Nakiete......
 Maji yakikatiza barabara eneo la ITV.....

 Mitungi ya Gesi ikielea kwenye maji.
Njia panda ya Kwa Mwalimu Nyerere.CHANZO KAJUNASON BLOG









PICHA ZAIDI ZA MAAFA YA MAFURIKO MAENEO MBALIMBALI

Chini na juu ni lori la mafuta likiwa limetumbukia eneo la Mbagala.
 Hatariiii......
 akijitutumua kupita lakini aaaah wapi, safari iliishia hapa.
 Hapa ni maeneo ya Kariakoo...
 Nje ya maduka ya Kariakoo leo mchana....
Huyu sasa hata sijui alikuwa akielekea wapi huku..
 Baadhi ya Nyumba zikiwa zimezungukwa na maji katika Eneo la Mzambarauni Mkoa wa Morogoro kutokana na Mvua zilizo nyesha.
Huyu jamaa anasubiri manusura.....hap jijini Dar
 Maji ya mvua yaliyosababisha mafuriko yakipita kwa kasi katika daraja la Mzambarauni mjini Morogoro.
Hapa ni eneo la Msasani jijini Dar....jamaa wakijaribu kuokoa baadhi ya mali zao walizofanikiwa kuwahi.
 Nyumba zikiwa zimezungukwa na maji....
Jamaa akiduwaa asijue la kufanya....
 Mtoto huyu akijitahidi kupunguza maji yaliyojaa ndani kwao kutokana na mvua zinazo endelea kunyesha na kusababisha mafuliko Mkoa wa Morogoro.
 Wakazi wa Morogoro wakipita ndani ya maji kutokana na Mvua kubwa iliyosababisha mafuliko leo.
 Nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa ikiwa imeezuliwa na upepo huku ikiwa imezungukwa na maji.
 Hatari tupu hapa hata wasafiri hawakuweza tena kuingia eneo hili kupata chochote kutokana na eneo hili kujaa maji.
Wakazi wa Morogoro wakiangalia baadhi ya nyumba zilizoezuliwa na upepo na kuzingirwa na maji.

No comments:

Follow by Email

DJ Luke Joe

DJ Luke Joe

PSPF

PSPF

MAAFA MENGINE JIJINI DAR ES SALAAM


Photo: scout Ally Juma on rescue missionPhoto: Member of Tanzanian scout association together picture with scout from Poland at Fire Rescue centre

Kumbe Mungu akiamua dar yote aigeuze beach inawezekana! acha kucheza na maji yana nguvu tosha! mie nahamia milima ya kitongaaaaa (18 photos)
Samuel Essau's photo.
jiji la dar es salaaam limezingilwa na maji skauti na vikosi vingine vinafanya kazi ya uokozi
Samuel Essau's photo.
jinsi gani vua ilivyo leta maafa katika mitaa ya watu mji umekuwa bwawa la kivutio la watarii
Like · ·

MAAFA MOROGORO

BAADA YA MAAFA YA LIYO TOKEA UKO MORO JE ? SKAUTI TULIFANIKIWA KWA KIASI GANI KUHAKIKISHA TUNAOKOA MAISHA YA WATU!
Picha za matukio ya maafa morogoro na tathmini.
8 April via HTC Sense
Murtadhwa El Bahsan's photo.
Baasda ya kuokoa baadhi ya wahanga wa maji na kupelekekwa kwenye hifadhi kwa ajili ya kupewa huduza za kijamii( kushoto ni kamishna wa skauti mratibu wa maafa taifa na mkoa kamishna juma masudi na kati na kulia ni watoo aambao pia ni waanga wa maafa huko morogoro wakisaidiana kufanya usafi katika kambi ya maafa.kichwa

Murtadhwa El Bahsan's photo.
Murtadhwa El Bahsan's photo.
Baasda ya kuokoa baadhi ya wahanga wa maji na kupelekekwa kwenye hifadhi kwa ajili ya kupewa huduza za kijamii( kushoto ni kamishna wa skauti mratibu wa maafa taifa na mkoa kamishna juma masudi na kati na kulia ni watoo aambao pia ni waanga wa maafa huko morogoro wakisaidiana kufanya usafi katika kambi ya maafa.
Murtadhwa El Bahsan's photo.
kamisha mkuu wa kikosi cha maafa taifa kamishna juma masudi akiwa anatoa maelezo ya juu ya athari za maafa

Wednesday, February 26, 2014

SHEREHE ZA KUMBUKUMBU YA KUZALIWA BADEN-POWELL ZAFANA



MAKAMISHNA WA SKAUTI MIKOA NA NAIBU WAO WAAPISHWA

 

Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwasisi wa Skauti Duniani Marehemu Baden-Powell zimefanyika katika nchi mbalimbali za Dunia.
Katika Jiji la Dar Es Salaam Sherehe hizo zilifanyika katika Kiwanja cha Kimataifa cha Biashara cha Mwalim Julius Kambarage Nyerere (Saba-Saba) barabara ya kilwa.
Shughuli hiyo iliyoandaliwa na Skauti Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kamati iliyoongozwa na Kamishna wa Skauti wa Mkoa huo Ndugu Abubakar Mtitu.


Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba (aliyevaa suti nyeusi) Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi, kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa tayari akisubiria maandamano ya Skauti, kulia ni Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akifuatiwa na Makamo Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Taifa Mzee Mwaking'inda (aliyevaa suti) na kushoto mwa picha ni Naibu Kamishna Mkuu ndugu Rashidi Mchatta. Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha kimataifa cha biashara cha Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Katika sherehe hiyo, Kamishna Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania (TSA) ndugu Abdulkarim Ismail Shah aliwaapisha Kamishna wa Mikoa na Manaibu wake.
Pia katika sherehe hiyo chama cha Skauti Tanzania kilizindua Mpango Mkakati wa Chama hicho.

Mgeni wa rasmi katika Sherehe hiyo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi Bi. Consolata Mgimba kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa alifika katika eneo la sherehe mnamo saa nne asubuhi tayari kwa kupokea maanamano na kuaza kwa sherehe hiyo.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akivishwa Skafu na Skauti tayari kupokea maandamano ya Skauti, tarehe 22 Februari 2014

Kamishna Mkuu wa Skauti Mheshimiwa Abdulkarim Shah, akizungumza baada ya salamu zake kwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baden-Powell.
Tarehe 22 Februari 2014 kaika kiwanja cha maonyesho ya kimataifa ya biashara cha  Mwl. Nyerere Dar Es Salaam.

Mgeni rasmi Bi. Consolata Mgimba Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi akitoa salamu kwa niaba ya Rais wa Chama ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Mheshimiwa Shukuru Kawambwa

Wednesday, February 19, 2014

RATIBA YA SHEREHE YA SIKU YA MWANZILISHI WA SKAUTI DUNIANI LORD BADEN POWEL - 22 FEBRUARI 2014



MUDA
TUKIO
MHUSIKA
Saa 3:00 Asubuhi
Skauti kuwasili Uwanja wa Taifa
Skauti wote
Saa 3:30 Asubuhi
Maandamano kuelekea viwanja vya Mwl. Nyerere, Saba Saba
Skauti na Viongozi wao
Saa 3:30 Asubuhi
Ø  Viongozi wa Chama kuwasili Ukumbini.
Ø  Skauti Mkuu na Mwenyekiti Kamati Tendaji(T)  kuwasili ukumbini.
Ø  Wageni waalikwa kuwasili ukumbini.
Kamati ya Mapokezi/ MC
Saa 4:00 Asubuhi
Mgeni Rasmi kuwasili Uwanjani na kuvishwa Skafu.
Ø  Mgeni Rasmi kupokea maandamano.
Kamishna Mkuu,
Naibu Kamishna Mkuu,
Kamishna wa Mkoa(DSM)
Kamishna Mtendaji,

Saa 4:05
Asubuhi
Mgeni Rasmi kuingia Ukumbini.
Ø  Wimbo maalum (Twamkumbuka Mzee wetu Baden Powell)
Ø  Utambulisho wa wageni maalum
Skauti wote


Kamishna Mkuu
Saa 4:15
Asubuhi
Nasaha za Skauti Mkuu
Skauti Mkuu
Saa 4:30 Asubuhi
Burudani
MC
Saa 4:40 Asubuhi
Uzinduzi wa Mpango Mkakati
(Strategic Plan 2014 – 2017)
Mgeni Rasmi,
Kamishna Mkuu Msaidizi Miradi.
Saa 4:50 Asubuhi
Kuapishwa kwa Makamishna wa Mikoa
Ø  Burudani.
Kamishna Mkuu
Skauti.
Saa 5:20 Asubuhi
Kuwekwa saini kwa Mkataba wa Hifadhi ya Msitu wa Vikindu
Kamishna Mkuu
Mkurugenzi wa Hifadhi ya Misitu
Saa 5:30 Asubuhi
Burudani (Maonesho ya Sanaa ya mapigano)
Kikosi cha Rova
Saa 5:40 Asubuhi
Tukio maalum

MC

Saa 5:50 Asubuhi
Nasaha za Mgeni Rasmi
Mgeni Rasmi
Saa 6:00 Mchana
Kurudia Ahadi
Wote/ Kamishna Mkoa
Saa 6:05 Mchana
Neno la shukrani
Mwenyekiti Kamati Tendaji
Saa 6:15 Mchana
Chakula
Kamati ya Chakula

MWISHO

Scout Law
  • Heshima ya Skauti ni kuaminiwa
  • Skauti ni mzalendo kamili
  • Skauti ni mtu wa kuwa faa wengine pia
  • Skauti ni rafiki kwa wote na ndugu kwa kila Skauti
  • Skauti ni mwenye adabu kamili
  • Skauti ni mwenye huruma kwa viumbe
  • Skauti ni mtiifu
  • Skauti ni mchangamfu daima
  • Skauti ni mwangalifu wa mali
  • Skauti ni safi katika mawazo, maneno, na matendo yake
Skauti si mjinga na mjinga sio skauti (ilisemwa na Baba wa Taifa Mwl. Nyerere)
  • A Scout's honnour is to be trusted
  • A Scout is loyal to his nation
  • A Scout is helpful to others
  • A Scout is friendly to all and a brother to every Scout
  • A Scout is courteous
  • A Scout is kind to all creatures
  • A Scout is obedient to his leaders
  • A Scout is always cheerful
  • A Scout is thrifty
  • A Scout is clean in thought, word and deed